Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa uongozi bora mijini ni tatizo katika ukuaji wa miji- UNHABITAT

Ukosefu wa uongozi bora mijini ni tatizo katika ukuaji wa miji- UNHABITAT

Hii leo ni siku ya kimataifa ya miji ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo ubunifu katika usimamizi wa miji sambamba na kuhakikisha inajumuisha kila mtu bila ubaguzi. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Makazi mijini yameendelea kuwa changamoto hasa katika nchi zinazoendelea… miji ikikua huku huduma zikizidi kufifia.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na makazi, UNHabitat linasema mwaka huu ikiwa ni mwaka mmoja tangu kupitishwa kwa ajenda ya maendeleo endelevu pamoja na mkutano wa tatu wa makazi ni vema kuhakikisha kuwa huduma upangaji wa miji unafanyika kwa usahihi ili ukuaji uwe endelevu na wakazi wake waishi maisha ya utu.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNHabitat, Joan Clos katika ujumbe wake anasema katika ukuaji wa miji huduma kama vile bustani za mapumziko, viwanja vya michezo na huduma nyingine za kijamii ni muhimu.

(Sauti ya Clos)

“Moja ya tatizo kwa nini katika baadhi ya maeneo hatufikii kiwango hiki cha utoaji huduma ni ukosefu wa uongozi bora. Ninadhani ni muhimu tuzingatie utendaji huu wa usimamizi bora. Bila usimamizi bora wa miji hakutakuwepo na hakikisho ya kwamba ukuaji miji utakuwa ukuaji sahihi unaotakiwa.”