Watu 12 wauawa katika shambulio la anga Libya:UNSMIL

31 Oktoba 2017

Watu 12 wameuawa na wengine saba kujeruhiwa katika shambulio la anga dhidi ya makazi ya raia eneo la Derna nchini Libya usiku wa kuamkia leo.

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL umelaani vikali shambulio hilo ambapo waliopoteza maisha ni wanwake na watoto na majeruhi pia wakihusisha watoto wanne.

UNSMIL imetuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na  kuwatakia majeruhi ahuweni ya haraka huku ukitoa wito wa kuwepo mara moja fursa ya misaada ya kibinadamu na kuondoa vikwazo vya kutembea hususani kwa watu wanaohitaji huduma ya matibabu.

Pia mpango huo umerejelea kauli yake kwamba mashambulizi ya moja kwa moja au ya kupangwa dhidi ya raia ni marufuku chini ya sheria za kimataifa na umezikumbusha pande zote kutekeleza wajibu wao wa kuwalinda raia.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter