Watu takriban milioni 3 wapata tiba ya Hepatitis C:WHO

31 Oktoba 2017

Watu takriban milioni 3 wameweza kupata matibabu ya homa ya ini aina ya C ( hepatitis C) katika kipindi cha miaka miwli iliyopita na wengine milioni 2.8 walianza 2016 matibabu ya muda mrefu ya homa ya ini aina ya B. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya homa ya ini iliyotolewa leo na shirika la afya ulimwenguni WHO kabla ya hapo kesho kuanza mkutano wa dunia wa homa ya ini nchini Brazil.

Akizungumzia kasi ya vita hivyo Dr Gottfried Hirnschall mkurugenzi wa WHO idara ya HIV na program ya kimataifa ya homa ya ini amesema wameshuhudia ongezeko la asilimi 5 la nchi zinazoendelea kuweka mipango ya kitaifa ya kutokomeza virusi vya homa ya ini katika miaka mitano iliyopita.

Ameongeza kuwa matokeo ya vita hivyo yanatia matumaini kwamba utokomezaji wa ugonjwa huo unaweza kutimia.

Mkutano wa dunia wa homa ya ini 2017 umeandaliwa na WHO na muungano wa kimataifa wa homa ya ini kwa hisani ya mwenyeji Brazil, lengo kuu likiwa ni kuzichagiza nchi kuchukua hatua kukabili homa ya ini ugonjwa ambao bado unakatili maisha ya watu zaidi ya milioni 1.3 kila mwaka na kuathiri wengine zaidi ya milioni 325.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter