Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kana kwamba vita havitoshi, njaa yaizogoma Kasai DRC:Beasley

Kana kwamba vita havitoshi, njaa yaizogoma Kasai DRC:Beasley

Njaa inalizonga jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambalo pia limeghubikwa na machafuko amesema mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpangio wa chakula duniani WFP.

David Beassley ambaye yuko ziarani nchini DRC tangu mwishoni mwa juma amesema robo ya watu wote ambao ni zaidi ya watu milioni tatu wana upungufu mkubwa wa chakula, huku kiwango cha utapia mlo uliokithiri kinazidi asilimia 10 ya kiwango cha dharura cha shirika la afya Ulimwengu WHO.

Asilimia kubwa ya watu milioni 1.4 waliolazimika kukimbia makwao wanaishi msituni au wamechukuliwa na familia ambazo pia zimezidiwa uwezo kutokana na mzozo unaoendelea.

Bwana Beasley amesema licha ya hali mbaya iliyopo mgogoro wa Kasai haujapewa uzito unaostahili, na msaada wa chakula wa WFP utamalizika Disemba hivyo ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza usaidizi.

Hivi sasa shirika hilo linajipanga kuwafikia watu 500,000 kwa msaada wa chakula  ifikapo Disemba na wengine wengi mwaka 2018.