Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi 1700 wa Rohingya wahamishiwa makazi mapya Bangladesh:UNHCR:

Wakimbizi 1700 wa Rohingya wahamishiwa makazi mapya Bangladesh:UNHCR:

Wakimbizi wapya 1700 wa Rohingya walioingia Bangladesh wamehamishiwa katika makazi mapya Kusini Mashariki mwa nchi hiyo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na hiyo kupunguza msongamano kwenye kambi ya Kutupalong.

UNHCR inasema wakimbizi waliohamishwa ni miongoni mwa maelfu ya wakimbizi ambao walisafiri karibu juma zima ili kuvuka mpaka na kuingia Bangladesh na kisha kukwama mpakani kwa siku nne kabla ya kuruhusiwa kuingia juma lililopita.

Shirika hilo limefungua kituo cha muda na baadhi ya shule za wakimbizi kwenye kambi ya Kutupalong ili kuwasaidia wakimbizi waliofurika kwa ghafla.

Kuhamishwa kwa wakimbizi hao kulianza Jumanne wiki hii na kumeruhusu shule kuanza tena na pia kutoa nafasi kwa akjili ya wakimbizi wapya wanaowasili.

Jumla ya wakimbiz 5000 watahamishiwa kwenye makazi mapya katika eneo la ekari 3000 lililotolewa na serikali ya Bangladesh.