Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Imbonerakure hawana uhusiano moja kwa moja na serikali Burundi- Tume

Imbonerakure hawana uhusiano moja kwa moja na serikali Burundi- Tume

Tume ya uchunguzi kuhusu Burundi leo imesema uchunguzi wao umebaini kuwa vijana wa Imbonerakure ambao wanadaiwa kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya raia nchini humo hawafanya kazi moja kwa moja na serikali.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani ambako wako kwa ajili  ya kuwasilisha ripoti yao mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wajumbe hao wamesema ingawa hawapokei maagizo moja kwa moja, vitendo vyao na yale wanayofanya yanakuwa yanatia wasiwasi.

Rais wa tume hiyo Fatsah Ouguergouz, ametolea mfano vitendo vya kutowesha watu, kukamata watu kinyume cha sheria na hata kufanya vurugu.

(Sauti ya Fatsah)

“Tumefikia hitimisho kuwa vitendo vya vijana hao haviwezi kuhusishwa moja kwa moja na serikali ya Burundi. Wanafanya mambo peke yao na watu hao hawahusishi kabisa watu wa serikali. Lakini wakati huo huo pengine vitendo vyao vinaweza kuhusishwa na serikali ya Burundi.”