Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zachukuliwa kukwamua elimu huko Manyara, Tanzania

Hatua zachukuliwa kukwamua elimu huko Manyara, Tanzania

Lengo namba nne la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linachagiza masuala ya elimu. Lengo hili linasaha hakikisho ya kwamba elimu inakuwa shirikishi na inakuwa pia bora kwa watu wote bila kujali jinsia, eneo aliko na hata rangi yake. Na kama haitoshi, Umoja wa Mataifa kupitia lengo hili, unataka elimu  hiyo siyo tu iwe bora elimu bali iwe elimu bora. Mantiki ya mtazamo huu ni kuhakikisha kuwa elimu inamwezesha mtu kukabiliana na maisha yake wakati wote wa uhai wake. Ni katika muktadha huo Yohani Gwangway wa radio washirika Radio SAUT FM ya Mwanza Tanzania ameangazia huko Babati, mkoani Manyara changamoto za elimu na jinsi ya kujikwamu.