Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa jimbo la HirShabelle Somalia aapishwa

Rais wa jimbo la HirShabelle Somalia aapishwa

Rais mpya wa jimbo la HirShabelle nchini Somalia Mohamed Abdi Waare, ameapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye mji wa Johwar nchini humo.

Rais WAaare alichaguliwa hivi  karibu ambapo katika hotuba yake ametoa wito kwa serikali ya shirikisho ya Somalia na majimbo yote kuheshimu mfumo wa shirikisho ambao amesema unakubalika nchini kote.

Amesema wanatumia mfumo wa shirikisho kama ulivyowekwa bayana kwenya katiba ya Somalia na kwamba kwa kuwa wameuchagua na uko kwenye katiba ni lazima wauzingatie.

RAis Waare amesema katu hawawezi kukubali kupingwa kwa mfumo wa shirikisho. Amesema ingawa kuna maoni tofauti, mjadala unaweza kuanzishwa ili kuweza kusonga mbele.

Rais Abdi Waare alichaguliwa kuwa rais wa jimbo la HirSabelle tarehe 16 mwezi uliopita wa Septemba baada ya mtangulizi wake Ali Abdullahi Osoble ambaye alishtakiwa na Bunge la jimbo hilo.

Uchaguzi na kuapishwa kwa Rais Waare kumeungwa mkono na Waziri Mkuu wa Somalia Ali Khayre ambaye amesema yuko tayari kushirikiana na serikali mpya ya jimbo la HirShabelle.