Leo ni miaka mitano ya huduma za IOM nchini Uturuki

26 Oktoba 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa Uhamiaji, IOM, leo linatimiza miaka mitano katika kutoa huduma kwa  zaidi ya wakimbizi milioni mbili kutoka kaskazini mwa Syria na nchi jirani,  waishio  Uturuki.

Mkuu wa IOM Uturuki, Lado Gvilava, amesema migogooro ya muda mrefu na mateso,  vimefanya mamilioni ya watu wanaokimbia unyanyasaji hawawezi kupata mahitaji au huduma za msingi.

Hivyo kupata fursa ya kuwahudumia kwa chakula, malezi, elimu ni jambo la msingi sana kwa binadamu.  Lado ansema ni wajibu wa shirika kuhahakisha binadamu hawa wanajengewa misingi ya matumaini ya maisha yao ya baadae.

Naye bwana Hiba ambaye ni  mkimbizi kutoka Syria anasema anashukuru  sana shirika la IOM kwa kumuezesha kupata kazi inayomsaidia kuhudumia familia yake.

Mnamo Septemba pekee, zaidi ya watu 190,000 walikimbia Syria, na kufanya idadi ya juma ya wakimbizi kufikia milioni sita, ambapo milioni  3.3 kati yao  wamekimbilia Uturuki na nchi jirani. Tangu 2015, mamilioni ya  wakimbizi wamefika kwenye pwani ya Ugiriki kutoka Uturuki na karibu 150,000 wameokolewa na walinzi wa Pwani ya Uturuki.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud