Maisha ya mamilioni ya watoto hatarini ,majira ya baridi kali:UNICEF
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhumia watoto UNICEF, limetoa wito wad ola milioni 60 kutoka kwa wahisani ili kusaidia kuokoa maisha yawatoto zaidi ya 1.5 katika majira yajayo ya baridi kali na theluji.
Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Mashariki , Kati na Afrika Kaskazini, Bw Geert Cappelaere amesema pesa hizo zitasaidia kuokoa maisha ya watoto wengi walioko katika nchini zilizoathirika na migogoro ya kivita kama Iraq, Syria, Palestina na nchi jirani, na pia watoto wanoishi katika kambi za wakimbizi ukanda wa mashariki na mashariki ya kati.
Aidha Bw Geert amesma bila msaada wa haraka, baridi inaweza kuwa pigo jingine kubwa kwa watoto walio katika mazingira magumu, akitolea mfano wa kupata magonjwa kama mfano ya kifua na pumu .
Hivyo amesisitiza upatikanaji wa pesa uatasaidia katika ununuzi wa blanketi, nguo za kuongeza joto na mafuta ya petroli kwajili ya genereta za kupasha joto.