Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilichosababisha kifo cha Dag Hammarskjöld bado ni kitendawili:

Kilichosababisha kifo cha Dag Hammarskjöld bado ni kitendawili:

Hatimaye ripoti ya tathimini ya mazingira yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld imewasilishwa kwa Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu Antonio Guterres.

Kwa kuzingatia azimio la baraza kuu nambari 71/260 mtu maalumu alipewa kujumu la kutathimini na kutoa hitimisho la hali na mazingira yaliyosababisha kifo cha Hammarskjöld na na watu alioambatana naona kisha nini kitakachofuata. Akifafanua kuhusu kilichojitokeza kwenye ripoti hiyo msemaji wa Katibu Mkuu, Farhan Haq amesema mtu aliyepewa jukumu la athmini hiyo amehitimisha katika ripoti yake kuwa

(FARHAN HAQ CUT 1)

“Ni dhahiri kwamba Dag Hammarskjöld na wajumbe alioambatana nao hawakuuawa baada ya kutua na kwamba abiria wote walikufa kutokana na majeraha waliyoyapata wakati wa ajali ya ndege, ama papo hapo, au muda mfupi baadaye.”

image
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld pichani mbele ya makau makuu wa Umoja wa Mataifa. Picha: UM
Na kuhusu sababu za ajali hiyo tathimini imebaini kwamba

(FARHAN HAQ CUT 2)

“Ni wazi mashambulizi ya nje au tishio linaweza kuwa sababu. Lakini pia amebainisha bado inawezekana kuwa ajali hiyo ilikuwa ni ajali inayosababishwa na kosa la rubani bila kuingiliwa msukumo wa nje, na kwamba sababu za kibinadamu ikiwemo uchovu vilihusika katika ajali.”

image
Dag Hammarskjöld na wafanyakazi wa UM wakishiriki katika sherehe ya Basi huko Vientiane, njia ya ya kuheshimu na kumtakia mema mtu yeyote. Anapokea bangili kutoka kwa wazee. Picha: UM
Kufuatia tathimini mtazamo wa Katibu Mkuu Guterres ni

(FARHAN HAQ CUT 3)

Taarifa iliyotolewa kwa Umoja wa Mataifa hadi sasa haitoshelezi kuhitimisha kuhusu sababu za ajali. Katibu Mkuu pia anafikiria kwamba inaonekana kuwa habari muhimu za ziada zipo.”

Katibu Mkuu ametoa wito kwa baraza kuu kuipitisha ripoti hiyo na hususan nchi wanachama kuendelea kutoa tarifa kuhusu kifo hicho. Amesisitiza kuwa ripoti hiyo ni hatua muhimu ya kuelekea kutimiza jukumu la pamoja la kupata ukweli wa nini hasa kilichotokea.