Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaongeza misaada ya dawa katika hospitali huko Ar-Raqqa

WHO yaongeza misaada ya dawa katika hospitali huko Ar-Raqqa

Kadri jimbo la Ar-Raqqa linavyoendelea kufikika baada ya magaidi wa ISIL kusambaratishwa, shirika la afya ulimwenguni, WHO linaendelea kuimarisha huduma zake kwa maelfu ya watu kwa kufikisha dawa na vifaa vya matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Al-Tabqa , kaskazini magharibi mwa  mji wa Ar-Raqqa.

Mwakilishi wa WHO nchini Syria, Elizabeth Hoff amesema msaada huo kutoka kwa wadau wake unalenga wakazi wa Ar-Raqqa vikisaidia matibabu kwa wagonjwa 500 wanaohitaji uangalizi mkuu kutokana na matatizo ya kiakili baada ya migogoro ya kivita.

WHO imesema hii ni mara ya pili wamefanikiwa kupeleka misaada ya dawa na matibabu katika Hospitali hiyo ya Al-Tabqa iliyofunguliwa upya mwezi uliopita na mpaka sasa wagonjwa 3400 wametibiwa wengi wa wakiwa  watoto .