Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

New Zealand yachangia dola milioni 1 kwa ajili ya ujenzi mpya Iraq: UNDP

New Zealand yachangia dola milioni 1 kwa ajili ya ujenzi mpya Iraq: UNDP

Serikali ya New Zealand imechangia dola milioni 1 katika wakfu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP (FFS) ambao unafadhili miradi ya ujenzi mpya katika maeneo ya Iraq yaliyokombolewa kutoka kwa kundi la wapiganaji wa ISIL.

Fedha hizo zinafanya mchango wa New Zealand kufikia leo kuwa ni dola milioni 2. Kufuatia vipaumbe vilivyoainishwa na serikali ya Iraq na mamlaka za maeneo husika FFS inasaidia kukarabati miundombinu ya umma , kutoa mikopo kwa wajasiriamali, kuinua uwezo wa serikali za mitaa, kuchagiza ushiriki wa raia na kutoa ajira ya muda mfupi kupitia miradi ya umma.

Kwa mujibu wa mratibu mkazi wa UNDP Iraq Lise Grand kiwango cha uharibifu Magharibi mwa mji wa Mosoul ni kibaya zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote nchini humo, na mifumo ya umeme, maji na maji taka yote inahitaji ukarabati.