Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ina mchango muhimu katika kutimiza ajenda ya 2030 kwa wakulima:FAO

Biashara ina mchango muhimu katika kutimiza ajenda ya 2030 kwa wakulima:FAO

Mikataba ya kimataifa ya biashara , viwango vya usalama wa chakula na hatua ambazo zinafaidisha balada ya kuathiri familia za wakulima katika nchi zinazoendelea ni lazima viwe malengo katika majadiliano ya ya kimataifa ya biashara.

Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO Jose Graziano da Silva leo katika mkutano wa maandalizi kwa ajili ya mkutano mkubwa wa mawaziri wa biashara utakaofanyika Desemba mjini Buenos Aires Agentina ukiwaleta pamoja maafisa kutoka serikali mbalimbali duniani.

Amesema miongoni mwa ajenda zitakazotamalaki ni biashara mtandaoni na kupanua wigo wa biashara ya kimataifa ya chakula kwani biashara ni muhimu sana katika mustakhbali wa wakulima na utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu au SDG’s.

(GRAZIANO CUT)

Ajenda ya mwaka 2030 inaitambua biashara kama kiungo muhimu katika kutimiza malengo mengi ya maendeleo endelevu. Na ni muhimu zaidi kwa lengo la pili la SDG’s la kutokomeza njaa na mifumo yote ya utapia mlo na pia katika kuchagiza uzalishaji na matumizi kama linavyosemwa kwenye lengo namba 12.”

Ameongeza kuwa lengo la jumla kwenye mkutano huo utakaoandaliwa na shirika la kimataifa la biashara WTO ni kutoka na matokeo ambayo yatakuwa hatua ya kwanza katika kuelekea ujumuishwaji, usawa na mifumo ya kimataifa yenye uwiano wa biashara.