Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Polisi wanawake wajenga imani ya raia Sudan Kusini

Polisi wanawake wajenga imani ya raia Sudan Kusini

Polisi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNPOL wamekuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha raia wanaishi salama. Mjini Juba, zaidi ya wakimbizi wa ndani 39,000 wanaishi katika maeneo ya ulinzi wa raia kwenye kituo cha Umoja wa Mataifa, na kama ilivyo katika miji mingine magenge ya wahalifu na uhalifu ni changamoto kubwa,  hususan ukatili wa kijinsia inayokumba wanawake na watoto wa kike.  Umoja wa Mataifa unasema polisi wanawake wana uwezo mkubwa wa kushirikiana na wanawake na watoto kwa njia rahisi, na hivyo jitihada za kuongeza wanawake katika ujumbe wake UNMISS zinaendelea, lengo kubwa likiwa ni kuimarisha uhusiano kati yao na raia. Katika makala ifuatayo, Selina Jerobon anaangazia jitihada za wanawake polisi nchini humo.