Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visa vya Polio vyapungua na sasa kuna nuru- WHO

Visa vya Polio vyapungua na sasa kuna nuru- WHO

Idadi ya visa vya ugonjwa wa polio vilikuwa ni vichache mwaka jana, ikilinganishwa na kipindi chochote kile tangu takwimu zimeanza kuchukuliwa.

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema hayo hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ugonjwa huo likiongeza kwamba taarifa hizi mpya ni nuru ya kwamba kuna mwelekeo wa kutokomeza kabisa polio duniani.

Mwaka jana pekee visa 12 ndio viliripotiwa katika nchi mbili ambazo ni Pakistan na Afghanistan huku Nigeria ikisalia kuwa ni miongoni mwa nchi tatu zilizoathirika zaidi na ugonjwa huo.

Yaelezwa kuaw kampeni za aina  yake na zenye ubora wa juu katika nchi hizo zimewezesha watoto kupatiwa chanjo na hivyo kuwaepusha dhidi ya ugonjwa huo unaosababisha vifo.

Christian Lindmeier ni msemaji wa WHO, Geneva, Uswisi.

(Sauti yaLindmeier)

"Ikiwa ni visa vichache zaidi vya polio kwa mwaka katika historia, ni ishara kuwa programu za kutokomeza ugonjwa zina fursa ya kipekee. Tangu mwaka 1998, maendeleo dhidi ya polio yamekuwa thabiti na endelevu huku visa vikipungua kwa zaidi ya asilimia 99 tangu kuanzishwa kwa mkakati wa kimataifa wa kutokomeza polio.Idadi ya watoto waliopooza kutokana na polio pori imepungua mwaka 2016, ikilinganishwa na wakati wowote ule katika historia ambapo kuliwa na visa 37 pekee.”

Hata hivyo licha ya kupungua kwa idadi ya visa vya polio, bado visa vipya vinagunduliwa kwenye maeneo ambayo ni magumu kufikika ambapo WHO inasema polio itasalia kuwa tishio kwa watoto endapo itaripotiwa popote pale.

image
Ugonjwa wa Polio husababisha watoto kupooza viungo, na pichani watoto wakipatiwa mafunzo ya kurejesha nguvu kwenye viungo vyao vilivyopooza. (Picha:http://www.unmultimedia.org/classics/)