Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasaidia wasomalia 134 kurejea nyumbani

IOM yasaidia wasomalia 134 kurejea nyumbani

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, limesaidia wakimbizi 134 wa  Somalia kurejea nyumbani kutoka Yemen.

Hatua hiyo ni katika kampeni iitwayo rejea nyumbani kwa hiari inayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya IOM na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR.

Wasomali hao ni wale waliokuwa wamekimbilia Yemen kusaka maisha bora na wakajikuta kwenye migogoro ya mara kwa mara ikiwemo unyanyasaji  katika kambi za wakimbizi ya Khares .

Miongoni mwao ni watu wazima 73 ambao wengi wao ni wanaume na wote walipatiwa pesa ya kujikimu pindi wanapowasili Somalia.

Mkuu wa IOM wa Yemeni Laurent de Boeck amesema  zoezi hili ambalo limetekelezwa tarehe 23 mweiz huu ni la tatu ambapo mmoja wa wanufaika Qasim Mohammed aliyeishi Yemen kwa miaka 25 na amesema ana furaha sana kurudi nyumbani.