Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usimlaumu mwalimu wakati mfumo ndio mbovu:UNESCO/ GEM

Usimlaumu mwalimu wakati mfumo ndio mbovu:UNESCO/ GEM

Msimlaumu mwalimu wakati mfumo wa elimu ndio mbovu na kuchangia changamoto zinazojitokeza katika elimu. Wito huo upo katika ripoti yam waka 2017/2018 ya ufuatiliaji wa elimu kimataifa GEM iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sanyansi na utamaduni UNESCO. John Kibego na taarifa kamili

(TAARIFA YA KIBEGO)

Ripoti hiyo inaeleza wajibu wa serikali kutoa elimu yenye ubora kwa wote na ikisisitiza kuwa uwajibikaji ni muhimu katika kufikia lengo hili, pi inaonya kwamba lawama isiyo ya kawaida kwa mhusika yeyote kwa matatizo ya elimu inaweza kuwa na madhara makubwa, kuongezeka pengo la kutokuwepo usawa na kuathiri kujifunza.

Akisistiza kuhusu hilo mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema “elimu ni jukumu la pamoja, kwa serikali, shule, waalimu, wazazi na sekta binafsi, na uwajibikali wa pande zote ndio utakaotoa muongozo wa jinsi walimu wanavyofundisha, wanafunzi wanavyosoma na serikali inavyochukua hatua.

Hivyo ameongeza ni lazima ipangwe kwa uangalifu, kwa kuzingatia misingi ya usawa, na ujumuishaji ili kufikia lengo la maendeleo endelevu namba 4 la elimu bora.

Ripoti hiyo imependekeza masuala manne kwa serikali zote duniani, mosi kuweka mfumo wa uwajibikaji kwa shule na waalimu, pili kuruhusu ushiriki wa kidemokrasia, tatu kuweka  sheria zinazowabana watoa elimu wa umma na binafsi, na nne kuifanya elimu kuwa ni haki kisheria.