Tanzania yapongeza usaidizi wa UM nchini humo

23 Oktoba 2017

Kuelekea siku ya Umoja wa Mataifa hapo kesho Oktoba 24, serikali ya Tanzania imepongeza mchango mkubwa wa chombo hicho katika kufanikisha maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa nchini Tanzania Dkt. Susan Kolimba ametoa pongezi hizo akihojiwa na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo, UNIC akitolea mfano usaidizi wa kifedha wa kupambana na ukatili wa kijinsia..

(Sauti ya Dkt. Susan)

Halikadhalika amezungumzia mpango wa usaidizi kwenye maeneo ya wakimbizi huko Kigoma akisema.

(Sauti ya Dkt. Susan)