Ujumbe wa amani kupitia midundo

20 Oktoba 2017

Suala la amani ni ndoto ya wengi katika nchi zinazoshuhudia mizozo huku mara nyingi raia wasio na hatia wakijikuta katika zahma ambayo hawakuitarajia.

Mzozo wa Somalia ambao umedumu kwa zaidi ya miongo miwili umesababisha Wasomali wengi kuwa wakimbizi na kuomba hifadhi katika nchi jirani.

Kilicho dhahiri ni kwamba raia wamechoka na vita na wangependa uwepo wa amani kwani faida zake ni chungu nzima.

Ni kufuatia azma hiyo ambao waimbaji kutoka Somalia wameungana kutuma ujumbe kuhusu amani kupitia muziki. Kwa undani zaidi basi ungana na Joshua Mmali katika makala hii.