Mwendokasi waleta nuru Dar es salaam, Tanzania

19 Oktoba 2017

Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania ni makao makuu ya kibiashara ya taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo kwalo bandari yake pia  hutumiwa na nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa. Mji huu una wastani wa ukuaji wa asilimia 7 kwa mwaka  kwa mujibu takwimu za Benki ya  Dunia .

Hata hivyo barabara mbovu, msongamano wa magari na ukosefu wa miondomibu ya usafiri unaoaminika ni kizingiti cha maendelao ya mji huu. Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia wamefanya kazi pamoja katika kuunda mfumo mpya wa mabasi ya mwendo kasi,  BRT, ili kurahisisha shughuli za maendelo kwa wakazi wa mji wa Dar es Salaam.  Je mfumo huo umeleta nuru ipi? Patrick Newman anasimulia katika makala hii iliyowezeshwa na Benki ya Dunia.