Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu barani Afrika iendane na mahitaji yetu- AU

Elimu barani Afrika iendane na mahitaji yetu- AU

Muungano wa Afrika umesema harakati za kujinasua katika lindi la umaskini barani zitafanikiwa iwapo elimu itakidhi mahitaji ya sasa.

Victor Harrison ambaye ni kamishna wa Tume ya Muungano wa Afrika, AU amesema hayo jijini New York, Marekani wakati akihutubia kikao cha ngazi ya juu cha jinsi ya kushirikisha vyema vijana ili kusongesha maendeleo ya Afrika.

Ikiwa ni katika kuadhimisha wiki ya Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, Kamishna Harissson amesema..

(Sauti ya Kamishna Harrison)

“Katika elimu mafunzo ya diploma pekee hayatoshi. Inahitaji kupata mafunzo ya ujuzi. Nini tunafanya baada ya masomo ya awali. Je tumechoka masomo au tuna uwezo wa kusonga mbele. Hilo ndio linafanyika kwetu. Tubadili elimu yetu iendane na mahitaji yetu.”

image
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mmoja wa vijana akiteka maji tayari kumwagilia bustani. (picha: Unifeed Video)
Kamishna Harrison akaenda mbali zaidi kuzungumzia ujasiriamali..

(Sauti ya Kamishna Harrison)

“Tunapaswa kuendeleza utamaduni wa ujasiriamali, tunapaswa kuendeleza ari ya ubunifu. Vijana wetu wana ari ya ubunifu kama vijana wengine. Je tunawasilikiliza? Je tunawapa wajibu? Je tunafanya hivyo? Hilo ndio swali.”

Amesema kando  ya kufikiria vitu vingine, Afrika iangazie kilimo hasa vijijini na kwamba iwahusishe vijana zaidi kwani wana uwezo mkubwa wa kujifunza mambo haraka.