Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ziara yangu CAR ni kuhusisha wadau ili kupunguza madhila kwa raia

Ziara yangu CAR ni kuhusisha wadau ili kupunguza madhila kwa raia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres ametangaza leo kwamba mapema wiki ijayo atazuru nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambako atasherehekea siku ya Umoja wa Mataifa  na mpango wa opresheni za amani nchini humo MINUSCA ili kuwawenzi walinda amani kote duniani.

(GUTERRES CUT 1)

“walinda amani wanaonyesha ujasiri mkubwa katika mazingira hatarishi na kujitolea kwa hali ya juu katika kuzisaidia nchi kuibuka kutoka katika migogoro.”

Tangu mwanzo wa mwaka huu walinda amani 67 wameuawa katika operesheni za Umoja wa Mataifa na 12 ni nchini CAR ambako hali ya usalama bado ni tete na hivyo katika ziara hii pia atahakikisha hali ya CAR ambayo haimulikwi sana na vyombo vya habari inatanabaishwa lakini pia.

(GUTERRES CUT 2)

Itakuwa ni fursa ya kushirikiana na Serikali na wengine ili kupunguza madhila, kuzuia kurudi nyuma kwa mchakato wa sasa, na kuimarisha msaada wa kimataifa kwa ajili ya amani.”

Pia amesema atalitupia jicho suala la unyanyasaji na ukatili wa kingono kwa kusistiza utekelezaji wa mtazamo uliochukuliwa na Umoja wa Mataifa kukomesha tabia hiyo.

(GUTERRES CUT 3)

Natiwa uchungu kwamba baadhi ya walinda amani wanadaiwa kutekeleza uhalifu huu wa unyanyasaji na ukatili wa kingono dhidi ya watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.”

Amesema hiki ni kipindi muhimu wa CAR, mengi yamefanyika ya mafanikio ikiwepo uchaguzi na kuwa na serikali lakini inahitajika kufanya kila liwezekanalo kulinda hatua hizo zilizopigwa.