UNFPA yatoa mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia kwa wathirika wa vimbunga

UNFPA yatoa mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia kwa wathirika wa vimbunga

Mjumbe maluum wa maswala ya ukatili wa kijinsia (GBV) wa  shirika la Umoja wa Mataifa la idadi wa watu ulimwenguni UNFPA, yupo ziarani katika visiwa vya  Antigua na barbuda kutoa mafunzo kwa watoa huduma na waathirika wa vimbunga wanaokabiliwa na ukatili wa kinjinsia kwenye makambi ya mpito.

katika mahojiano na UN News  Bi verena Bruno ambaye ni mtaalamu wa mswala ya ukatilia wa kijinsia, amesema sababau ya kuwepo kwake katika visiwa hivyo ni pamoja na kusaidia serikali za nchi hizo katika kutoa mafunzo kwa jamii ya visiwa hivyo ili kukabiliana na tatizo la ukatili wa kijinsia haswa kwa waathirika wa vimbunga ambao kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao, wanalazimika kuishi kwenye makambi ya mpito.

(Sauti ya Vereno)

Kama sehemu ya usaidizi wetu tumefanya tathmini haswa katika makambi ya mpito  kwenye visiswa vya barbuda ambako waathirika wa vimbunga wengi wamehifadhiwa, tumebaini kwamba kuna umuhimu wa kuwafunza watoa huduma, wanaume kwa wanawake  jinsi ya kuishi na kufanya kazi katika misingi ya kuepuka unyanyapaa au ukatili wa kijinsia makambini .

Hatua zipi ,watoa huduma kwenye makambi ya mpito wanatakiwa kuchukua ili kuzingatia usalama wa waathirika walioko makambini?

(Sauti ya Vereno)

Tunaongozwa na kanuni zilizopamgwa na  kamati kuu ya shirika kuhusu ukatili wa kijnsia. Ni muhimu sana kanuni hizi  kuzingatiwa na kila ngazi za uongozi kwenye makambi ya mpito mara tu huduma zinapoanza na zitakapofungwa. Tuna hahakikisha kua uongozi unazifahamu hizi kanuni na kuzitekeleza.