Ushiriki wa baba mtoto anapozaliwa una faida zake

17 Oktoba 2017

Ni kawaida barani Afrika kushuhudia mama anapotaka kujifungua kuwa hospitali peke yake, tofauti na mataifa mengi yaliyoendelea ambapo baba ana nafasi yake katika kushuhudia mwanae akizaliwa. Nchini Uganda mambo yameanza kubadilika na wanaume wametambua umuhimu wa kuwa sanjari na kina mama au wake zao wanapojifungua. Kwa undani zaidi ungana na mwandishi wetu John Kibego katika makala hii ya wanawake na uzazi nchini humo.