Wakimbizi na wahamiaji waendelea kushikiliwa mateka Libya
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, linaendelea na jitihada za kusadia mahitaji ya dharura kwa wakimbizi zaidi ya 14,500 wanaosadikiwa kutekwa na magenge ya wahalifu katika maeneo mbalimbali ya mji wa Sabratha huko Libya .
Bwana Andrej Mahecic ambaye ni msemaji wa UNHCR, akizungumza leo Mjini Geneva amethibitisha kupata taarifa kutoka serikali ya Libya kuwa zaidi wahamiaji 6,000 wamendelea kutekwa na wahalifu katika maeneo mbalimbali nchini humo. Amesema hii inafanya jumla ya idadi ya wahamiaji Sabratha kufikia 20,500, ikiwa ni pamoja na wale walio katika vituo vya uhamiaji.
UNHCR imekua mtari wa mbele kutoa misaada ya dharura katika maeneo yote ambako wakimbizi na wahamiaji wamehamishiwa, na wanaendela kufanya tathmini kuhusu mahitaji mengine kwa wahamiaji hao.
Halikadhalika UNHCR imetoa malori 15 yaliyosheheni misaada ikiwa ni pamoja na mikeka ya kulala, magodoro, vifa vya kujisafi na blanketi za baridi.
Serikali ya Libya kwa kushirikiana na UNHCR na washirika wengine wanaendela kutoa misaada mbalimbali ya dahurua japo uwezo wa kuwahudumia ni mdogo ikilinganisha na mahitaji ya wahamiaji hao.