Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tushikamane tutokomeze umaskini- Guterres

Tushikamane tutokomeze umaskini- Guterres

Leo ni siku ya kutokomeza umaskini duniani ambapo maudhui ni kujibu wito wa Oktoba 17 mwaka 1992 wa kutokomeza umaskini uliotokana na azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Akizungumzia siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres ametaka mshikamano zaidi ya watu milioni  800 duniani walio katika maisha ya ufukara.

Amesema kama hiyo haitoshi, wengine wengi hawana ajira, hawafahamu mustakhbali wao, ukosefu wa usawa umewazingira huku mabadiliko ya tabianchi yakizidi kuwatumbuza kwenye shida.

Kwa mantiki hiyo amesema lazima kuzingatia ajenda 2030 ya maendeleo endelevu ambayo….

(Sauti ya Guterres)

“Ahadi yake ya kutomwacha mtu nyuma itahitaji mbinu bunifu, ubia na suluhu.”

Hivyo akasema..

(Sauti ya Guterres)

“Hii ina maana kushughulikia mzizi wa umaskini ili kuutokomeza kabisa. Inamaanisha kusikiliza maoni na mwongozo wa watu wanaoishi kwenye umaskini na kwenda nao sambamba. Hebu na tushikamane na tutokomeza umaskini kwa utu.”

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, watoto ndio wameathirika zaidi na ufukara ambapo mtoto yuko katika hatari zaidi ya kuishi kuwa maskini mara mbili zaidi kuliko mtu mzima.