Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kimataifa njaa imeongezeka kwa mara ya kwanza baada ya muongo:FAO

Kimataifa njaa imeongezeka kwa mara ya kwanza baada ya muongo:FAO

Idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani imeongezeka kwa mara ya kwanza baada ya muungo na kufikia watu milioni 815 duniani , limesema leo shirika la chakula na kilimo FAO.

Tangazo hilo limeenda sanjari na wito wa baba mtakatifu Francis wa kuzitaka serikali kushughulikia suala la uhamiaji uliosababishwa na kutokuwepo uhakika wa chakula unaohusishwa na mabadiliko ya tabia nchi na vita.

Wito huo umeungwa mkono na afisa wa FAO mjini Geneva Uswis Bi Carolyn Rodrigues-Birkett, anayeanza kwa kueleza FAO na washirika wake wanachukua hatua gani kushughulikia mizizi ya tatizo hilo hasa vijijini.

(SAUTI YA CAROLYN)

“Ni lazima tuongeze juhudi zetu mara mbili kwa sababu idadi ya watu walio na lishe duni imeongezeka kutoka milioni 777 hadi milioni 815, baada ya tatizo hilo kupungua kwa miaka mingi. Hii inasababishwa na kuongezeka kwa migogoro na athari za mabadiliko ya tabia nchi na mdororo wa uchumi katika baadhi ya sehemu duniani.”