Nitapaza sauti yangu zaidi baada ya matumaini ya elimu kwa wakimbizi: Muzoon

16 Oktoba 2017

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Muzoon Almellehan amekwenda nchini Jordan ili kukutana na watoto ambao kama yeye walikimbia machafuko Syria na sasa wamejizatiti kwenda shule licha ya mazingira ya changamoto yanayowakabili.

Hii ni mara ya kwanza Muzoon  amerejea Jordankatika nchi ambayo aliishi miaka mitatu kama mkimbizi kambini kabla ya kwenda kuunganishwa na familia kwa kupewa makazi nchini Uingereza mwaka 2015.

Baada ya kuwasili Jordan na kukutana na watoto wenye matumaini ya elimu amesema ametiwa moyo wa kupaza sauti yake hata zaidi kwa ajili ya watoto milioni 27 ambao hawako shuleni, ambao sauti zao zimenyamazishwa na kwa muda mrefu na fursa zao za kupata elimu  na matumaini yako ya kuwa na msiaha bora yamesambaratishwa na vita.

Takriban watoto milioni 2.4 wa Syria hawapati elimu wakiwemo milioni 1.7 ndani ya Syria na wengine zaidi ya 730,000 wakiwa ukimbizini Misri, Jordan, Lebanon na Uturuki