Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhamiaji uwe wa hiari na si shuruti- Papa Francis

Uhamiaji uwe wa hiari na si shuruti- Papa Francis

Leo ikiwa ni siku ya chakula duniani, tukio maalum limefanyika kwenye makao makuu ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO huko Roma, Italia ambapo kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis ametaka serikali duniani kote kushirikiana ili kuhakikisha uhamiaji unakuwa ni salama na jambo la hiari si shinikizo. Taarifa zaidi na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Makao makuu ya FAO, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Graziano da Silva akiingia ukumbini na mgeni wake Papa Francis…

Nats…

Video maalum ikachezwa kuonyesha madhila ya uhamiaji na athari zake kwa chakula…. Watu kutoka nchi mbalimbali Afrika, Asia, Ulaya wakilazimika kuhama kwa sababu ya vita, njaa na ukame…

Mkurugenzi Mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva akasema mamilioni ya watu wanahama makwao na idadi inaongezeka kila uchao..

(Sauti ya Da Silva)

“Idadi kubwa ya watu hao wanahama kwa sababu ya mizozo na mabadiliko ya tabianchi. Na wengi wao wako tayari kuhatarisha maisha yao kupitia jangwa la Sahara na  hata baharí ya mediteranea.”

Naye Papa Francis akasema ni wazi kuwa vita na mabadiliko ya tabianchi yanasababisha njaa kwa hiyo jamii ya kimataifa isichukulie kwamba njaa ni jambo lisilokuwa na tiba.

(Sauti ya Papa Francis)

“Ni muhimu kuwa na mjadala wa hiari ili kumaliza mizozo na pia kuazimia kwa dhati kuondokana na silaha kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Matifa na pia hatua dhidi ya usafirishaji wa silaha.”

Ametaka kuwepo kwa mfumo thabiti wa kutokomeza kabisa silaha na kubadilika mfumo wa maisha sambamba na matumizi bora ya rasilimali ili kulinda sayari ya dunia.

Kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wananchi wanasemaje siku ya chakula?

(Sauti ya Furaha)