Utegemezi wa bidhaa unadhoofisha uchumi wa nchi zinazoendelea
Kamati Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD imetoa ripoti leo mjini Geneva Uswis , ikihusu utegemezi wa nchi tisa zinazoendelea katika mauzo ya nje ya bidhaa kati ya mwaka 2010 na 2015, na kufanya idadi ya nchi hizo kufikifkia 91, ambayo ni theluthi mbili ya nchi 135 zinazoendelea.
Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Utegemezi wa mapato ya Serikali inaonyesha kwamba, nchi zinazoendelea zimeshuhudia mapato ya mauzo yakiongezeka 25% hadi kufikia $dola trilioni 2.55.
Naye katibu mkuu wa UNCTAD Bw. Mukhisa Kituyi amesema, nchi zinazoendelea zitakuwa na wakati mgumu kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu zisipoachana na tabia ya utegemezi wa bidhaa zinazosafirishwa nje.
Ameongeza kuwa utegemezi wa bidhaa unaweza kuathiri vibaya viashiria vya maendeleo ya kibinadamu kama vile umri wa kuishi, elimu, na mapato ya kila mtu, kwa mujibu ripoti ya utegemezi wa bidhaa ya 2016, karibu theluthi mbili ya nchi zinazoendelea zimerekodiwa katika kutegemea bidhaa zinazosafirishwa nje mwaka 2014 hadi 2015.
UNCTAD inafafanua kuwa nchi inafikia hatua ya kuwa tegemezi kwa bidhaa wakati bidhaa zake za kuuza nje zinachukua zaidi ya asilimia 60 ya mauzo ya jumla ya bidhaa.