Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kutoa msaada wa dharura wa chakula kwa wakimbi wa ndani

WFP kutoa msaada wa dharura wa chakula kwa wakimbi wa ndani

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula (WFP) limeanza kutoa msaada wa chakula kwa familia zilizohamishwa na mapigano  ya makundi ya waasi katika mji wa  Sabratha  Magharibi ya Libya.

Mkurugenzi wa WFP Lybia bw. Richard Ragan amesema tangu mwishoni mwa Septemba, watu zaidi ya 15,000 wamehamia miji iliyo karibu na mji wa Sabratha.

WFP na washirika wake wameanza kutoa chakula kwa  wakimbizi wa ndani wapatao 1,500 ambao wameathiriwa sana na mapigano , na  kila mgawo wa chakula  unatosha kwa falimia ya watu 5  ukijumuisha  tambi, unga wa ngano, maharage, mafuta ya kupikia, sukari na nyanya.

Aidha WFP imsema mapigano ya wenyewe kwa wenyenye nchini Lybia yameathiri mfumo wa maisha ya watu hivyo hufanya raia kuhitaji misaada ya mashirika ya kibinadamu.

WFP inalenga kuwasaidia Walybia  175,000 walio katika hali ngumu huku ikitoa  kipaumbele kwa familia zilizoathiriwa na migogoro ya kivita.