Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Niger inapiga hatua katika mfumo wa kutoa tahadhari kuhusu mafuriko

Niger inapiga hatua katika mfumo wa kutoa tahadhari kuhusu mafuriko

Kila mwaka mvua nyingi husababisha mafuriko nchini Niger ambapo tangu mwezi Juni mwaka huu watu 56 wamepoteza maisha na wengi zaidi wameathirika.

Hiyo ni kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani na usalama wa umma nchini humo sababu kubwa ikielezwa kuwa ni kutokuwepo na mbinu za kutoa tahadhari ya mapema na kukabiliana na hali hiyo.

Ni kwa mantiki hiyo shirika la hali ya hewa duniani WMO, Benki ya Dunia pamoja wataalamu wa masuala ya hali ya hewa, maji na usalama wa chaukula wanakutana nchini  Niger kuanzia tarehe 9 mwezi huu hadi kesho Ijumaa kusongesha mpango wa kutoa tahadhari mapema na hatari za mabadiliko ya tabianchi kwa lengo la kuhakikisha utayari wa Niger katika kukabiliana na hatari ifikapo mwaka 2020.

Mradi huo  uliopatiwa jina CREWS unafadhiliwa na Australia, Ufaransa, Ujerumani, Luxembourg na Uholandzi huku WMO na Benki ya Dunia wakiwa ni wadau.