Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na Serikali ya Bangladesh kusaidia ujenzi wa vyoo kwa warohingya

UNICEF na Serikali ya Bangladesh kusaidia ujenzi wa vyoo kwa warohingya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ,UNICEF na Wizara ya Usimamizi wa Maafa na Usaidizi ya Serikali ya Bangladesh wamekubaliana kujenga vyoo 10,000 katika kambi ya  warohingya iliyoko wilaya ya Cox ya Bazar ili kuzuia kuzuka kwa magonjwa .

Makubaliano hayo yametiwa saini kati ya mwakilishi wa UNICEF Bangladesh Edouard Beigbeder na katibu mkuu wa wizara  ya  usimamizi wa mafaa Muhammad Habibul Kabir  ambapo ujenzi utagharimu dola za kimarekani milioni 1.5.

Vyoo  hivyo vitakavyonufaisha watu 250,000 vitajengwa na wanajeshi wa Bangladesh ambapo kila choo kinagharimu dola 157.

Bwana Biegder amesema tayari wamepokea taarifa kutoka vituo vya afya kambini hapo kuhusu uwepo wa magonjwa yatokanayo na ukosefu wa huduma za kujisafi.

Amesema UNICEF watatoa msaada unaohitajika wa kifedha na kiufundi ili kufanikisha azma ya wizara hiyo ya afya.