Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkakati wa kimataifa wa uhamiaji ujikite na watu, uhakikishe usalama na utu kwa wote-Arbour

Mkakati wa kimataifa wa uhamiaji ujikite na watu, uhakikishe usalama na utu kwa wote-Arbour

Mchakato unaojumuisha serikali mbalimbali ili kupitisha mkakati wa kimataifa kwa ajili ya usalama, utu na mpangilio kwa ajili ya wahamiaji unaendelea leo mjini Geneva Uswisi.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji wa kimataifa Bi Louise Arbour amezungumza katika mkutano huo na kusema wakati mchakato mzima wa kupitisha mkakati wa kimataifa kwa ajili ya wahamiaji unaongozwa na nchi wanachama, ushirikishwaji wa wadau wengine kama asasi za kiraia ni muhimu ili kuupa uhalisia mjadala huo.

Ameongeza kuwa asasi za kiraia ni mahali pazuri pa kubaini mapengo na mapungufu katika majadiliano ya nchi wanachama na kuunda masuala ambayo yataleta tija katika mchakato huo.

Bi Arbour amesisitiza kwamba ili kufanikiwa mkakati huo wa kimataifa ni lazima ujikite na watu ili kuhakikisha usalama na utu kwa wote.

Kesho tarehe 12 ndio itakuwa siku ya mwisho ya sehemu ya sita ya mjadala huo kuhusu uhamiaji wa kimataifa na uhamiaji wa masuala yanayohusiana na ajira.