Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wimbi la Warohingya latarajiwa tena Bangladesh:UNHCR

Wimbi la Warohingya latarajiwa tena Bangladesh:UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, kwa kushirikiana na serikali ya bangladesh wanajiandaa kupokea umati mkubwa wa wakimbizi wanaokimbia mauaji ya wenyewe kwa wenyewe  yanayolenga kabila la wa Rohingya nchini Myanmar.

UNHCR, imethibitisha taarifa kutoka kwa vikosi vya ulinzi vya Bangladesh mpakani kuhusu wimbi la warohingya 11000 waliovuka mpaka jana wakisaka hifadhi Bangladesh, ambapo wengi wao wametoka eneo la Buthidaung kilomita 25 mashariki mwa Maungdaw, kaskazini  mwa jimbo la Rakhine Myanmar.

UNHCR imesema , miongoni mwa  wambizi  walionusurika kuuaua  baada ya kutembea kwa zaidi ya siku 14 ni watoto na  akina mama , ambapo alikuwepo mvulana mmoja aliyeonekana akiwa na jeraha kubwa shingoni mwake.

Aidha UNHCR kwa kushikiana shirika la mpango wa chakula duniani WFP, shirika la kuhudumia watoto UNICEF, shirika la uhamiaji IOM, shirika la afya duniani WHO, kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC na ACF wameendelea kutoa huduma za dharura za  chakula, maji na  afya  kwa wakimbizi wapya .

wakati huohuo tume ya serikali ya Bangladesh ya wakimbizi (RRR) imekubali kutenga ardhi na kuanzisha vituo vidogo vya usaidizi katika veneo la mapokezi  ili kutoa maji na tahadhari za dharura za matibabu kwa wakimbizi wapya.