Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washtushwa na kutekwa kwa mfanyakazi wa misaada Darfur:

UM washtushwa na kutekwa kwa mfanyakazi wa misaada Darfur:

Mratibu mkazi na masuala ya kibinadamu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan amesema ameshtushwa sana na kitendo cha kutekwa nyara kwa mfanyakazi wa misaada ya kibinadamu kutoka Uswis mnamo Jumamosi ya Oktoba 7 kwenye jjimbo la Darfur Kaskazini.

Bi Marta Ruedas ameelezea hofu yake baada ya kutekwa kwa Bi Margaret Schenkel akisema kuwalenga wahudumu ambao wako hapo kwa ajili ya kutoa misaada ya kibinadamu ya kuokoa Maisha ni uhalifu chini ya sheria za kimataifa.

Amezitaka pande zote nchini Sudan kuhakikisha Bi Margaret Schenkel anaachiliwa akiwa salama. Tarehe 7 Oktoba watu wasiojulikana wakiwa na silaha walimteka Margaret nyumbani kwake El-Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini.

Hili ni tukio la tatu la kutekwa kwa muhudumu wa misaada ya kibinadamu jimboni Darfur katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.