Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yatoa msaada wa dharura kwa wahamiaji Sabratah Lybia

IOM yatoa msaada wa dharura kwa wahamiaji Sabratah Lybia

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, limetoa  msaada wa dharura huko Sabratah Libya, kilometa 80 magharibi mwa mji mkuuTripoli kwa wakimbizi 4000  wanoajaribu safari za hatari za kwenda Ulaya kutipitia Bahari ya Mediterania

Othman Belbeisi ambaye ni mkuu wa IOM Libya amesema baada ya migogoro ya wenyewe kwa wenyewe nchini  humo kusababisha  kutokua na kituo maalumu kwa muda mrefu, IOM imefanikiwa kuhamishiawakimbizi  kwenye kambi ya hangar kwenye mji wa Dahman.

Ameongeza kuwa IOM ilifanikiwa kuorodhesha wahamiaji 2,600 kwenye mtandao wao ambapo 1,819 ni wanaume, 704 wanawake na watoto 77 kwajili ya kupewa huduma ya chakula na afya.

Anasema wahamiaji walioshikiliwa wametoka katika nchi kumi na mbili na miongoni mwao ni wanawake wajawazito, watoto wachanga na watoto wasio na wazazi. Hivyo timu ya matibabu ya IOM inafanya tathmini ya  mahitaji ya afya , ambapo tayari mwanamke mmoja majamzito alihamishiwa kwenye kliniki ya kibinafsi, kilomita 10 kutoka Sabratah, na kujifungua mtoto salama.

Halikadhalika IOM imewapa fursa wahamiaji kurudi nyumbani  kwao kupitia mpango wake wa usaidizi wa kurudi kwa hiari. Wakati huo huo  serikali ya  Libya imetoa tamko la kuwahamisha  wahamiaji  hao kutoka tripoli  na tayari, wahamiaji wapatao 2,000 wako katika mchakato wa kuhamishwa  na DCIM na IOM.