ICRC yapunguza shughuli zake Afghanistan

9 Oktoba 2017

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC, imeamua kupunguza shughuli zake nchini Afghanistan  baada ya mfululizo wa mashambulizi  dhidi ya wafanyakazi wake  kaskazini kwa nchi hiyo. 

Hii  ni mujibu wa Monica Zanareli ambaye ni mkuu wa ujumbe wa ICRC nchini Afghanistan ambaye amesema tangu mwezi Disemba mwaka 2016 vituo vya ICRC kaskazini mwa Afghanistan, vimeshambuliwa mara 3. 
 
Amesema baada ya majadiliano na makao makuu ya shirika hilo huko Geneva, ICRC sasa ofisi za ICRC huko Maimana na Kunduz zitagungwa na kupungunza  uwakilishi wake huko Mazar-i-Sharif .
 
Bi Zanareli amesema  uamuzi  wa kupunguza shughuli zao Afghanistan umekua mgumu kwao baada ya miaka 30 ya huduma  ya  shirika hilo nchini.
 
Miongoni mwa visa vilivyokumba ICRC nchini Afghanistan ni pamoja na mfanyakazi wake kutekwa nyara mwaka 2016 huko Kunduz, na kuachiwa huru baada ya wiki 4.
 
Tukio hili lilifuatiwa na mauaji ya kikatili ya wafanyakazi sita  kuchinjwa na wengine wawili kutekwa nyara katika jimbo la Jawzjan. 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter