Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yasihi nchi zaidi zijiunge na mkataba wa kupinga uvuvi haramu

FAO yasihi nchi zaidi zijiunge na mkataba wa kupinga uvuvi haramu

Nchi zote duniani zimetakiwa kujiunga na mkataba wa makubaliano ya bandari ya nchi kwa ajili ya kuunga mkono mkataba wa aina yake unaolenga kukabiliana na uvuvi haramu kama mbinu ya kutokomeza uhalifu huo unaoigharimu dunia mabilioni ya dola na kuharibu lishe na mazingira.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva katika kongamano la bahari huko Malta akiongeza kuwa nchi zote zinahitajika kuwa sehemu ya mkataba huo ili uwe na mafanikio.

Bwana Graziano Da Silva ameongeza kwamba kufikia sasa nchi 50 zimeridhia mkataba lakini nyingi zaidi zinahitajika.

FAO kwa sasa inaongeza maradufu juhudi zake za kutekeleza mkataba huo na imejitolea kifedha kwa ajili ya kusaidia nchi masikini kuwekeza katika teknolojia, sayansi na sheria zinazohitajika.