Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya kutokomeza nyuklia yashinda tuzo ya amani ya Nobel

Kampeni ya kutokomeza nyuklia yashinda tuzo ya amani ya Nobel

Taasisi ya kimataifa inayoendesha kampeni dhidi ya matumizi ya silaha za nyuklia imeshinda tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2017, hatua ambayo imepokelewa kwa mikono miwili na Umoja wa Mataifa. Flora Nducha na taarifa kamili.

(Taarifa ya Flora)

Berit Reiss-Andersen, Mwenyekiti wa kamati ya Nobel ya Norway akitangaza kuwa kamati yao imeamua kutunuku tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2017 kwa taasisi inayofanya kampeni ya kimataifa ya kutokomeza silaha za nyuklia, ICAN.

Uamuzi huo umezingatia jinsi ICAN inaangazia madhara ya silaha za nyuklia duniani na mafanikio ya kupitishwa kwa mkataba wa kutokomeza silaha hizo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza hatua hiyo kupitia akaunti yake ya twitter.

Naye Linnet Ngayu  kutoka baraza la viongozi wa dini barani Afrika ACRL- nchini Kenya, wadau wa ICAN amezungumzia walivyopokea taarifa hizo..

(Sauti ya Linnet)

Na je wao kupokea tuzo hiyo kunatuma ujumbe gani?

(Sauti ya Linnet)