Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unyanyapaa kwa wenye VVU bado kikwazo cha kupata huduma : UNAIDS

Unyanyapaa kwa wenye VVU bado kikwazo cha kupata huduma : UNAIDS

‘‘Pale watu wanoishi na HIV, au walio katika hali hatarishi ya kupata HIV, wanaponyanyapaliwa katika vituo vya afya, wanadidimia. Hili kwa hakika hudhoofisha juhudi zetu za kuwafikia watu wenye HIV kupima, kutibiwa na huduma za kuzuia’’ Amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mapambano dhidi ya Ukimwi UNAIDS, Michel Sidibé

Akizindua ripoti mpya kuhusu unyanyapaa dhidi ya waathirika wa VVU iitwayo Kuukabili ubaguzi: Tokomeza unyanyapaa dhidi ya HIV na ubaguzi katika huhuma za afya na kwingineko mjini Geneva Uswis, Bwana Sidibé amesema inatoa ushahidi na vidokezo vya namna ya kukabiliana na unyanyapaa na ubaguzi ili kuhakiikisha walengwa wanapata huduma za afya.

Ripoti inaonyesha kuwa watu wanaoishi na VVU ambao hukumbwa na kiwango kikubwa cha unyanyapa wanakabiliwa na hatari ya kuchelewa kupata huduma za afya mara mbili kuliko wale ambao hawanyanyapaliwi. Bofya hapa kwa taarifa http://bit.ly/2yETTGZ