UNHCR yahitaji msaada wa dharura wa zaidi ya milioni 83 kusaidia Warohingya

6 Oktoba 2017

Shirika la  Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limetangaza ombi la msaada wa dharura wa dola milioni 83.7  kwa  ajili ya kusaidia mahitaji ya kiusalama kwa wakimbizi  zaidi ya laki 5 wa rohingya walioko nchini Bangladesh.

Msemaji wa UNHCR Andrej Mahecic  amesema, msaada huo wa dharura utakaoelekezwa kwenye kambi za Kutupalong na Nyapara, utalenga ulinzi wa wakimbizi, makazi, maji na usafi wa mazingira na pia kuimarisha uwezo wa wenyeji wa kusini-mashariki mwa Bangladesh ambao wanasaidia wakimbizi hao.

Ameongeza kuwa idadi kubwa ya wakimbizi ni wanawake, wazee na watoto ambao wengi wao hawajaambatana na familia zao au wametengana na familia zao.

Hata hivyo UNHCR imesema ingawa bado pesa zinahitajika kukidhi mahitaji ya dharura ya mwezi septemba 2017 hadi Februari ya 2018, wanachukua fursa kushukuru mashirika ya misaada na serikali ambazo tayari zimesaidia.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter