Kampeni ya kutokomeza Malaria ishirikishe wananchi- Dkt. Winnie

Kampeni ya kutokomeza Malaria ishirikishe wananchi- Dkt. Winnie

Nchi 8 zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, zimechukua hatua za kipekee ili kuondokana na ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030. Nchi hizo kupitia wakuu wa  nchi zao wameazimia kwa kufanya yale ambayo yanaonekana ni magumu. Mathalani kutenga bajeti ili kukidhi mahitaji ya kukabiliana na Malaria. Halikadhalika, kwa kuzingatia kuwa ni nchi jirani, basi wana ushirikiano kuhakikisha kuwa kutokomeza malaria nchi moja haiwi chanzo cha kuhamishia ugonjwa huo nchi nyingine. Nchi hizo ni Botswana, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe wakipatia ubia awo #Elimination8. Lakini je nini wamefanya? Leo tunaangazia Swaziland ambapo Dkt. Winnie Mpanju Shumbusho, mwenyekiti wa ubia wa kutokomeza Malaria duniani, RBM amemweleza Assumpta Massoi wa idhaa hii hatua zilizochukuliwa.