Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuta ya mbogamboga yapiga jeki bei ya vyakula-FAO

Mafuta ya mbogamboga yapiga jeki bei ya vyakula-FAO

Bei ya vyakula imepanda kwa mwezi Septemba kwa mujibu wa orodha ya bei ya vyakula ya shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO.

Orodha hiyo inaonyesha ongezeko la asilimia 0.8 ikilinganishwa na mwezi Agosti  na asilimia 4.3 ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka jana.

FAO inasema mafuta ya mbogamboga ndio yaliyochangia ongezeko hilo ambapo bei yake imeongezeka kwa asilimia 4.6 hususani mafuta ya mawese , soya na alizeti.

Pia bidhaa za maziwa zimeongezeka kwa asilimia 2.1 ukilinganisha na mwezi wa Agosti zikiongozwa na siagi na jibini wakati kukiwa na matatizo ya usambazaji wake nchini Australia, New Zealand na kwenye mataifa ya Muungano wa Ulaya.

Hata hivyo orodha hiyo inaonyesha hakukuwa na mabadiliko yoyote ya bei kwenye bidhaa za nyama.