Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaume wana nafasi kubwa kufanikisha elimu kwa mtoto wa kike- Malala

Wanaume wana nafasi kubwa kufanikisha elimu kwa mtoto wa kike- Malala

Mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa Malala Yousafzai amesema wanaume wana nafasi kubwa katika kusaidia watoto wa kike kufanikisha ndoto yao ya kupata elimu. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Malala ambaye ni alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka jana wa 2016, ameiambia Idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuwa nafasi ya mwanaume katika elimu ya mtoto wa kike ni dhahiri kwa kuwa wasipofanya hivyo ndoto za watoto wa kike zinazimika.

Ametolea mfano wa baba yake mzazi ambaye dada zake watano hawakuweza kwenda shule lakini aliazimia kuwa lazima binti yake mmoja wa kike ambaye ni Malala lazima aende shule licha ya ugumu uliokuwepo kwenye makazi yao huko nchini Pakistan.

(Sauti ya Malala)

"Kwa hiyo wanaume wanapaswa kujitokeza, wanapaswa kusaidia wanawake. Ni manufaa kwa uchumi mzima na pia kwa kila mmoja wetu. Itasaidia uchumi kukua haraka, na pia kuboresha kiwango cha maisha kwa kila mmoja wetu. Itaboresha afya. Itasaidia pia watoto kwa sababu iwapo wanawake wataelimisha wanakuwa katika fursa nzuri ya kulea watoto wao, elimu yao na mustakhbali wao."

image
Malala Yousafzai akijibu swali toka kwenye hadhara huku Katibu Mkuu António Guterres akitazama, ni wakati wa moja ya vikao kwenye Umoja wa Mataifa. (Picha: UN/Rick Bajornas)
Alipoulizwa ni kitu gani kinampatia nguvu kila uchao, Malala amesema kuwa amepitia mambo mengi ikiwemo ugaidi na vitisho..

(Sauti ya Malala)

“Na sasa baada ya kuponea chupuchupu kuuawa, uhai nilio nao sasa una malengo na kusudio hilo ni elimu kwa watoto. Tunaishi kati ya miaka 70 hadi 80 na kwa nini maisha hayo yasiwe kwa malengo bora? Kwa nini tusitumie maisha kutoa huduma ya kiutu ambayo itasaidia dunia.?”