Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaomba dola milioni 120 kusaidia wakimbizi wa Rohingya

IOM yaomba dola milioni 120 kusaidia wakimbizi wa Rohingya

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji limetoa ombi la dola takriban milioni 120 kwa ajili ya kuwasilisha misaada ya dharura kwa wakimbizi zaidi ya laki tano wa kabila la Rohingya kutoka Myanmar ambao wamewasili wilaya ya Cox's Bazar nchini Bangladesh.

Kumiminika kwa wakimbizi kwa makumi ya maelfu wa jamii ya warohingya walioanza kukimbia machafuko jimbo la Rakhine nchini Myanmar kumesababisha hali ya dharura kwenye eneo hilo.

IOM imetoa ombi hilo kwa ajili ya mahitaji ya kuanzia Septemba 2017 hadi Februari 2018 kama sehemu ya mpango wa uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.