Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNCHR yaonya kuhusu ukiukwaji wa haki za wakimbizi

UNCHR yaonya kuhusu ukiukwaji wa haki za wakimbizi

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limeonya vikali kuhusu  Ukiukwaji wa sheria za kimataifa za wakimbizi, unaofanywa  na askari kushambulia familia zinazokimbia katika hali ya kuokoa maisha yao mipakani. 

Onyo hilo lipo katika ripoti ya leo iliowasilishwa  huko Genevia Uswisi na Bw.Volker Türk ambae ni Kamishina mkuu msaidizi  wa UNHCR kuhusu ulinzi wa wakimbizi , kwenye mkutano wa kila mwaka wa Kamati ya utendaji wa shirika hilo.

 

Katika ripoti hiyo wataalamu hao wamejumuisha mauaji ya wakimbiziyanayofanywa na  wanajeshi ambayo yanazidi kuongezeka ikiwemo matukio makubwa ya wakimbizi kuvamiwa usiku wa manane na  na mara kwa mara kulazimiswa kurejea katika nchi zao  za asili.

Halikadhalika Bwana Turk alisema vitendo hivyo havina madhara kwa wakimbizi pekee bali pia kwa jamii nzima kwa ujumla. Ameongeza kua hali hiyo inawathiri  wakimbizi milioni  22.5 duniani amabapo mwaka jana , watoto 64,000waliotenganishwa na wazazi wao walipatikana mpakani mwa  Marekani  na Mexico .

 Amesema  kama Umoja wa Mataifa tunao wajibu wa kufungua upya mjadala wa kile kilichokuwa kizuizi cha ulinzi wa kimataifa kwa miongo saba na kuhahakikisha mamilioni ya wakimbizi ambao wanategemea mfumo huu hawana wasiwasi kuhusu usalama wa maisha yao.