Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya waRohingya huenda ukawa ukiukaji wa haki za binadamu-Wataalam

Ukatili dhidi ya waRohingya huenda ukawa ukiukaji wa haki za binadamu-Wataalam

Kamati ya kuondoa unyanyasaji dhidi ya wanawake CEDAW, na kamati ya haki za mtoto CRC zimetoa wito kwa mamlaka nchini Myanmar kumaliza mara moja ukatili katika jimbo la Rakhine Kaskazini na kufanya uchunguzi wa haraka na kuwashitaki wale wanaotekeleza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Taarifa ya wataalam wa Umoja wa Mataifa imeelezea masikitiko yao kuhusu hatma ya wanawake na watoto ambao wako katika hatari ya ukiukaji wa haki zao, ikiwemo mauaji, kubakwa na kulazimishwa kuhama.

Kwa mujibu wa taarifa yao vitendo hivyo vinavyotekelezwa na jeshi na mamlaka ya usalama ambapo wanawake na watoto ndio waathirika vinaweza kuwa ukatili dhidi ya binadamu.

Ili kuhakikisha uwajibikaji kamati hizo zimetoa wito kwa serikali ya Myanmar kutoa fursa na kushirikiana na ujumbe wa kufanya utafiti ulioanzishwa na baraza la haki za binadamu kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

Hatimaye wameitaka mamlaka Myanmar kushughulikia mahitaji ya wakimbizi wa ndani wa jamii ya Rohingya na wale wanaoishi kambini katik nchi jirani kwa ushirikiano na jamii ya kimataifa.