Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubaguzi na unyanyapaa ni kikwazo cha vita dhidi ya ukimwi:UNAIDS

Ubaguzi na unyanyapaa ni kikwazo cha vita dhidi ya ukimwi:UNAIDS

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS limeonya kwamba ubaguzi na unyanyapaa vinazuia watu walioathirika na ukimwi kupata huduma muhimu za afya.

Ripoti mpya iliyochapishwa leo na shirika hilo inaonyesha jinsi gani unyanyapaa na ubaguzi ni vikwazo katika kuzuia, kupima, na kupata huduma ya tiba ya HIV na hivyo kuweka maisha ya mamilioni ya watu katika hatari kubwa.

Ripiti hiyo “kubabiliana na ubaguzi:kuzuia unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya HIV katika mafumo wa huduma za afya na zaidi, imezinduliwa na mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michel Sidibé, wakati wa kongamano la kijamii la baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswis.

Ripoti inaonyesha pia watu wanaoishi na HIV na kukabiliwa na unyanyapaa wa hali ya juu wako katika hatari ya kuchelewa mara mbili zaidi kujiandisha katika huduma za afya kuliko wale wasio nyanyapaliwa.

Takwimu za ripoti hiyo zinaonyesha kuna nchi 19 ambako mtu mmoja kati ya wanne wanaoishi na HIV wamepitia unyanyapaa. Michel Sidine ni mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS anasema

(SAUTI YA SIDIBE1)

“Katika baadhi ya nchi zaidi ya asilimia 40 ya watu waliobadili jinsia wanakwepa kutafuta huduma za afya kwa sababu ya jinsi walivyo. Watu wanaoishi na virusi vya HIV wanaoogopa unyanyapaa kwa sababu ya sheria za unyanyasaji, na tuna nchi 70 zinye sheria za unyanyasaji, wanakimbia. Tunashuhudia watu wengi zaidi wanaojidunga sindano za dawa za kulevya wakijificha , wakiendelea kuambukiza wenzi wao kwa sababu hawawezi kujitokeza kusaka huduma za afya. "

UNAIDS inasema wakati watu wanaoishi na HIV wakisubiri hadi wawe wagonjwa sana kuweza kupata huduma za afya , inakuwa vigumu dawa za kupunguza makali ya ukimwi kufanya kazi inavyopaswa.

Ripoti imependekeza kwamba dunia inahitaji kusimama kidete kuukabili ubaguzi na unyanyapaa ili kuwafikia watu wote kwa matibabu ili kunusuru Maisha ya wengi.